Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alan Ritchson: Mpiga picha alitaka kunishambulia kingono

AlanRitchson (1).jpeg Alan Ritchson

Sun, 7 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muigizaji wa Filamu, Alan Ritchson na Staa wa Mfululizo wa movie ya #Reacher amefunguka stori yake kipindi ni mwanamitindo na sababu zilizompelekea kuachana na fani hiyo.

Ritchson alikuwa mwanamitindo ambapo alikuwa akifanya kazi na makampuni kama #Abercrombie & Fitch na #CalvinKlein alisema sababu iliyompelekea kuachana na kazi hiyo ni baada ya Mmoja ya wapiga picha maarufu kutaka kumshambulia kingono.

Katika mahojiano mapya na #TheHollywoodReporter, #Ritchson anasema kuna siku alitumwa na kampuni yake kukutana na mpiga picha maarufu (Jina hakutaja) katika chumba cha hoteli ili kupiga picha za uchi huku akimuahidi atakuwa mstari wa mbele kwenye magazeti makubwa.

Anasema baada ya muda Bwana huyo alimvamia na kumshambulia Kingono lakini alitoka kwa hasira na kwenda mpaka kwenye kampuni yake na kuwafokea kisha kuacha kazi kwani hakupendezwa na kitendo hicho.

Ritchson alisema kuwa tasnia hiyo imezungukwa na matukio ya namna hiyo na nikama yameshahalishwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live