Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alama za vidole za Tupac, Biggie zaingizwa sokoni

Notorious X BIG Alama za vidole za Tupac, Biggie zaingizwa sokoni

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kadi zenye alama ya vidole vya waliokuwa wasanii wa muziki wa hip-hop marehemu Tupac na Biggie walizosaini baada ya kukamatwa kwao zaingizwa sokoni.

Alama hizo zinauzwa na Wafanyabiashara Wakuu wa Kumbukumbu za Kitaifa kwenye mtandao wa Momentintime.com, kwa gharama ya dola 225,000 kwa kila moja ambazo ni zaidi ya tsh 564.4 milioni.

Kadi yenye alama za vidole vya Tupac ilitokana na kukamatwa kwake mwaka 1995 kutokana na kupatikana na hatia ya unyanyasaji wa kingono na kumpiga shabiki wa kike anayeitwa Ayanna Jackson jambo lililopelekea ahukumiwe jela kifungo cha mwaka mmoja na miezi mitano lakini alitumikia kifungo hicho kwa miezi 9.

Aidha kwa upande wa Biggie kadi hiyo ni ya mwaka 1995 kwa kesi yake ya wizi na shtaka la unyanyasaji aliofanya Pennsylvania hata hivyo mashtaka ya wizi yalitupiliwa mbali baadaye.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live