Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Al Pacino kupata mtoto wa nne akiwa na umri wa miaka 83

Muigizaji Marekani Kupata Mtoto Wa Nne Akiwa Na Umri Wa Miaka 83 Muigizaji Marekani kupata mtoto wa nne akiwa na umri wa miaka 83

Wed, 31 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwigizaji Al Pacino anatarajia mtoto wake wa nne akiwa na umri wa miaka 83, wawakilishi wake wamethibitisha.

Nyota huyo wa 'Godfather' ametangaza kwamba mpenzi wake Noor Alfallah mwenye umri wa miaka 29 ana ujauzito wa miezi minane.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya Marekani Pacino na Alfallah wamekuwa pamoja tangu janga la Covid-19.

Pacino tayari ana watoto watatu - wawili na Beverly D'Angelo na mmoja na Jan Tarrant.

Katika kazi yake iliyochukua zaidi ya miongo mitano, Pacino ameonekana katika filamu za The Irishman, The Godfather, Scarface na Scent of a Woman, akishinda tuzo ya Oscar kwa mwigizaji bora kwa filamu ya mwisho.

Alfallah anafanya kazi katika tasnia ya filamu na ametoa filamu kama vile Billy Knight, Little Death na Brosa Nostra.

Hapo awali alichumbiana na mwanamuziki Mick Jagger mnamo 2017.

Mwigizaji mwenza wa Pacino kutoka The Godfather Part II, Robert de Niro,hivi majuzi alitangaza kuwa amemkaribisha mtoto wake wa saba akiwa na umri wa miaka 79.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live