Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akothee kwenye penzi zito na mzungu "Mahaba yanizike!"

Ef Akothee

Fri, 23 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwimbaji na mjasiriamali mashuhuri Esther Akoth almaarufu Akothee anaonekana kuyafurahia sana mahusiano yake mapya.

Mama huyo wa watoto watano ameendelea kudokeza kuwa tayari ana mpenzi mpya baada ya kutengana na Nelly Oaks. Hata hivyo bado hajafichua sura au jina la mwanaume ambaye ameuteka moyo wake kwa sasa.

Siku ya Jumamosi Akothee alipakia picha na video kadhaa zilizoonyesha akiwa likizoni mjini Mombasa. Wakati huo alikuwa kwenye kundi la watu wasiotambulishwa.

"Chakula cha mchana Mombasa...Mama yangu ananisubiri kanisani," aliandika chini ya video alizopakia kwenye Instastori.

Katika video moja, mwanaume mzungu anayeaminika kuwa mpenziwe mpya alisikika akimwambia, "Endelea kumsubiri mama yako."

Katika video iliyofuata Akothee anaonekana akimbusu mzungu huyo huku akiwa ameficha uso wake. Mikono ya mwanaume huyo asiyetambulishwa mieupe ilionekana ikiwa imemkumbatia shingoni.

"Uuuwi mapenzi nouwe, mahaba inizike," Akothee aliandika chini ya video hiyo.

Katika chapisho lingine, msanii huyo alidokeza kuwa tayari amekubali ndoa na mzungu huyo. Walikuwa wameweka dau kwamba ikiwa mpenziwe angefanikiwa kumwangusha chini basi iwe ishara kuwa amekubali.

"Sawa basi, ni Ndio... Mtu amwambie mamangu atoke tu kwa kanisa aende nyumbani nilienda kwa date ya chakula cha mchana Mombasa kidogo," Aliandika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live