Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akothee azungumzia madai ya kutengana na mumewe 'Omosh'

Akothee Azungumzia Madai Ya Kutengana Na Mumewe 'Omosh' Akothee azungumzia madai ya kutengana na mumewe 'Omosh'

Wed, 4 Oct 2023 Chanzo: Radio Jambo

Mwimbaji Esther Akoth almaarufu Akothee amejibu madai yanayovuma kwenye mitandao ya kijamii kwamba ameachana na mumewe Denis ‘Omosh’ Shweizer.

Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 43 alikuwa akishiriki mazungumzo na mtaalamu wa urembo Kristeen Kuria alipowazungumzia watu wanaodai kuwa ndoa yake imevunjika.

Katika video aliyoichapisha kwenye akaunti yake ya Instagram, Akothee alisikika akishangaa kwa nini watu wanadai kuwa ameachana na mume wake mzungu ilhali yeye mwenyewe bado hajasema.

“Na kwa nini wanadhani tumeachana? Ata sijasema tumeachana! Sijasema tumeachana na wameanza kuniambia ndio ‘Ojingo wa 8’,” alisikika Akothee akisema kwenye video hiyo.

Mama huyo wa watoto watano aliendelea kutania kuwa harusi nyingine inakuja hivi karibuni akisema kuwa bwana harusi wake ajaye ataitwa ‘Bw Ojingo.’

“Kuanzia leo, mimi ni Bi Ojingo. Ojingo ni jina la muda tukiwa bado tunamtafuta bwana harusi. Unapomwona tu bwana harusi anayefuata, ni ‘Ojingo’. Ita polisi," alisema.

Mwanamuziki huyo pia hakukosa kuwaonya watu wanaojifanya kumjali dhidi ya kumpigia simu wakitaka kujua zaidi akibainisja kwamba hana deni la maelezo kwa mtu yeyote nje ya safu yake ya watu wa karibu.

Uhusiano wa sasa wa Akothee na mumewe Denis Shweizer haujulikani wazi kwani bado hajatoa taarifa rasmi kuhusu hali ya ndoa yao. Hata hivyo, kumekuwa na tetesi nyingi kwamba ndoa hiyo haipo tena na kwamba hawako katika maelewano mazuri.

Vitendo vya hivi majuzi kwenye mitandao ya kijamii vimezidisha tetesi za kuachana huku wanamtandao wakiwa na shauku kubwa ya kupata majibu.

Chanzo: Radio Jambo