Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akothee azawadia gari la Sh mil 131 la kupelekea mtoto kliniki

Car Akothee 1024x576 Akothee

Tue, 4 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki Esther Akoth almaarufu Akothee amefichua kuwa gari alilozawadiwa na mpenzi wake Mzungu, Schweizer  siku chache zilizopita liligharimu shilingi milioni 6.8 za Kenya (sawa na Tsh milioni 131) ni la kupeleka mtoto kliniki.

Akothee alisema kuwa pesa hiyo ni kidogo sana kwake na wala sio kitu cha kuwafanya watu kupiga kelele.

Mama huyo wa watoto watano amesema kwamba anahisi vyema kudekezwa na kutunzwa kwani amezoea kujifanyia mambo.

"Ni mchakato wa kufikiria unaonipunga mimi,ni kitambo kupokea zawadi . Nilikuwa nimechoka na kujitunza, sasa hii ya kupeleka mtoto clinic imekuwa kesi,"alisema.

Mwanamuziki huyo alisema kuwa mzungu wake anampenda na pia alimshukuru Bw Schweizer upendo na kumzawadi gari hilo.

Akothee na mzungu wake wamekuwa kwenye mahusiano kwa muda mchache sasa. Mwimbaji huyo alimfichua mpenzi wake mpya mwezi uliopita, miezi kadhaa tu baada ya kutengana na Nelly Oaks.

Akothee amekuwa akidokeza kufunga pingu za maisha na mzungu wake hivi karibuni na hata kutafuta waandaaji wa harusi.

Baadaye alifichua kuwa  Dr Ofweneke anamtoza shilingi milioni 1.4 ili kufawidhi hafla ya harusi yake.

"Wee nilidhani tulikuwa marafiki na @drofweneke, ananichaji 1.4 m kuwa MC rasmi mnamo siku ya harusi yangu, ya kizungu na ya kitamaduni," alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Katika chapisho lake la huo wakati, Akothee alikiri kuwa hajawahi kuhisi vizuri jinsi anavyohisi sasa akiwa kwenye mahusiano yake mapya na Bw Schweizer na kujigamba kupata mzungu mdogo kuliko wazungu ambao ameweza kuwa kwenye mahusiano nao.

"Wee kama angekua guka ,zile matusi ningepokea , ni Mungu tuu. Mungu wa Akothee akupate pia. Nakupenda mpenzi❤," alisema katika chapisho lingine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live