Mtayarishaji mkongwe Suge Knight ameibuka na tuhuma nzito dhidi ya Mwanamuziki na Mfanyabiashara AKON, kwamba aliwahi kumbaka binti wa miaka 13.
Kwenye mahojiano na David Mayers kupitia Podcast yake mpya ‘Collect Call’ Suge Knight alisema bifu yake na Akon haikuwa kwa sababu ya pesa, bali tukio la kumbaka binti huyo wa miaka 13 ambaye ni mtoto wa rafiki yake.
Suge Knight ameeleza kwamba, Akon pamoja na mtayarishaji wake wa muda mrefu aitwaye Detail walifanya tukio hilo ambapo kulikuwa na binti mwingine mwenye miaka 12 ambaye Detail naye alimfanyia ukatili huo wa Kijinsia.
Baada ya kugundulika hilo, dada wa binti huyo alitaka kwenda polisi lakini kutokana na ukaribu ambao Suge alikuwa nao kwa Akon, ilibidi amshauri wayamalize tu.