Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akon: Najutia kumsaidi Olamide

Akon Ges (12).jpeg Akon na Olamide

Wed, 20 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wahenga na akili yao kubwa iliyokuwa mbele ya muda wametufunza daima kuwa ‘Majuto ni Mjukuu”. Hivi ndivyo mwanamuziki mkongwe Ulimwenguni ‘Akon,’ ameelezea masikitiko yake kwa kutomsaini rapa wa Nigeria ‘Olamide Adedeji’ miaka kadhaa iliyopita.

Katika mahojiano ambayo amefanya mkali huyo wa ndudo la “Blame It On Me” amepepeta maneno kuwa kiongozi wa Lebo ya YBNL Nation, ‘Olamide’ a.k.a‘Baddo,’ ndie mwanamuziki ambae alikuwa anayempenda sana wakati huo.

‘Akon’ ameonyesha majuto hayo na kudai kuwa pengine ningesema “Nilipokutana nae kwa mara ya kwanza nilimwambia Olamide, ndiye msanii ninayempenda sana. ndiye Mnigeria ambaye natamani ningesaini naye kabla ya yeye kujianzishia lebo yake ya YBNL’.

Huenda ‘Olamide’ angekuwa chini ya lebo ya ‘Konvict Kulture’ ya ‘Akon’ kusingempa njaa yakuikuza lebo yake ya YBNL, ambayo ni moja ya lebo kubwa sana barani Afrika inayowasimamia wanamuziki kama ‘Fireboy DML’ na ‘Asake’.

Hivi karibuni Rapa na mwimbaji huyo wa Nigeria, amefungukia kuwa maamuzi yake ya kuanzisha lebo hiyo yametokana na kushindwa kuzitumia pesa zake nyingi zinazotokana na muziki wake, akafanya maamuzi ya kusaini wanamuziki wapya ili azitumie huko kama sehemu yakurudisha kwa jamii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live