Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akon: Mafanikio yananiwezesha kubaini asili yangu Afrika

Akon Wake Wengi Msanii Aliaune Damala Bouga Time Puru Nacka Lu Lu Lu Badara Akon Thiam.

Fri, 1 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa RnB, Aliaune Damala Bouga Time Puru Nacka Lu Lu Lu Badara Akon Thiam maarufu kama Akon amekuwa kwenye biashara ya muziki kwa takriban miaka 20. Na mwimbaji huyo wa mwenye uraia wa Senagal na Marekani anasema hatimaye ameweza kuanza kujitengenezea muziki.

Mwanamuziki huyo ambaye alizaliwa Marekani Marekani, katika maisha yake ya utotoni alikuwa akiishi maisha yake kwa kuhama kati ya New Jersey na nchi hiyo ya Kiafrika.

Alijifunza kucheza ala kadhaa za muziki za magharibi na Afrika, lakini alipoanza taaluma ya muziki mapema miaka ya 2000, anasema watayarishaji walivutiwa tu na upande mmoja wa urithi wake.

"Moja ya mambo makubwa ambayo nililazimika kujitenga nayo wakati nilijitokeza kimuziki, ni ukweli kwamba nilikuwa Mwafrika," aliiambia BBC Newsbeat.

"Hilo halikuwa jambo ambalo wangeweza kuliuza au kukuza katika aina hiyo ya uwanja ambao nilikuwa nikichezea."

Kibiashara, Akon alipata mafanikio makubwa, akipata umaarufu mkubwa katika nyimbo za pop na RnB kama vile Lonely na Locked Up.

Lakini anasema mahitaji ya kifedha ya biashara ya muziki, na hitaji la kupata pesa, vilikuwa na athari kwenye pato lake.

"Kila kitu kilipaswa kuhesabiwa," anasema. "inachosha na unaanza kujisikia kama unafanya kazi."

Tangu apate mafanikio hayo ya awali nyota huyo wa Smack That amebuni lebo yake ya kurekodi, na kuanzisha biashara kama vile maduka ya nguo zake kwa jina Konvict Clothing.

Baadhi ya miradi yake - kama vile kujenga "Real life Wakanda" nchini Senegal kwa kutumia sarafu yake ya cryptocurrency - haijakamilika kama ilivyopangwa.

Lakini anasema imetosha kumfikisha katika nafasi ambayo hategemei tena watu wengine kumuunga mkono.

Kufanya kazi ya muziki akiwa na umri wa miaka 50 kunatokana zaidi na "shauku na mapenzi kwa muziki", anasema, na anaweza kujumuisha "ushawishi zaidi wa Kiafrika" katika kazi yake kwa sababu hakuna shinikizo kubwa kwake la kutafuta pesa.

"Muziki sio chanzo changu cha kwanza cha mapato kwa sasa, umeshuka hadi labda wa kumi," anasema.

Anasema uhuru wa kifedha unamaanisha kuwa anaweza "kuongeza utamaduni zaidi" kwa nyimbo zake, na anasema nyimbo zake mpya za Afro Freaks EP ni "mageuzi makubwa" zikilinganishwa na Lonely na Locked Up.

"Naweza kufurahia kuifanya bila kujishughulisha na siasa, na biashara ya muziki inayoambatana nayo," anasema.

EP mpya ya Akon imetungwa sana kwa ladha ya Afrobeats - aina ambayo imekuwa maarufu duniani kutokana na wasanii kama Davido, Wizkid na Burna Boy.

Anasema amekuwa akijaribu kukuza mtindo wa muziki, ambao unachanganya mvuto wa Kiafrika na Magharibi, kwa miaka mingi, na hata kumsaini Wizkid kwa lebo yake mwenyewe mnamo 2008.

Lakini Akon anakumbuka wakati ambapo Afrobeats ingepuuziliwa mbali na wakuu wa sekta muziki ya Marekani.

"Nakumbuka huko nyuma mwanzoni mwa miaka ya 2000, nilipokuwa nikijaribu kutafuta soko na kupata saini ya Afrobeats huko Amerika, walidhani ni muziki wa Reggae," anasema.

"Ilikuwa moja ya mambo ambayo yalikuwa ya kukatisha tamaa, kujaribu kuwafanya waelewe idadi ya Waafrika ilikuwa kubwa, na muziki huu utakuwa siku zijazo.

"Kwa bahati mbaya, nilipata shinikizo kubwa."

Ingechukua miaka 10 zaidi kabla ya Afrobeats kufanikiwa kabisa, huku wasanii wakubwa kama vile Drake na Beyonce wakishirikiana na nyota wakubwa wa Afrobeats.

Na wakati Wizkid alipotwaa Tuzo ya Grammy mwaka wa 2021, Akon anasema ilikuwa "mojawapo ya zile 'nilikuambia mara nyingi' wakati huo".

Anasema kupanda kwa Afrobeats kumetokana na kizazi kipya "kuwa wadadisi zaidi kuhusu muziki mpya unaowazunguka".

"Na nadhani mitandao ya kijamii ilikuwa na jukumu kubwa katika kupanua sauti za aina tofauti, kwa sababu hatukuwa na majukwaa yoyote," anasema.

Mafanikio ya kama vile ya Davido Ulaya "yalibadilisha mienendo" kwa wasanii wa Afrobeats, Akon anasema, na kuwapa wazo bora zaidi la jinsi ya kukabiliana na Marekani.

Anasema kwamba uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa Waafrika wenzake ulisaidia "kueneza nyimbo zake", kwa "kunyakua machapisho hayo yote" ya mitandao ya kijamii na "kufichua Afrobeats" kwa njia fulani.

Akon anasema: "Kila mtu anafanya sehemu yake, kujaribu kuufanya ulimwengu kuona ni kitu gani. Na mara walipoona waliupenda sana , unajua?

"Hiyo ndiyo iliyobadilisha kila kitu."

g Na anadhani hali ya baadaye ya muziki wa Afrobeats ni nzuri

"Afrobeats itakuwepo kwa muda mrefu, kwa sababu imekuwepo kwa muda mrefu [tayari]," anasema.

"Jukumu ambalo nililifanya kwa kweli lilikuwa kusaidia kuifichua, kuiweka nje, na kutumia kila fursa niliyokuwa nayo, na kila uhusiano niliokuwa nao, kila rasilimali niliyokuwa nayo, kuitambulisha na kutumaini kwamba watu watavutiwa."

Na Akon anaamini kwamba itachochea udadisi kuhusu bara lake la nyumbani, na wasanii wapya hawatalazimika kujitenga na mizizi yao kama yeye.

Afrobeats "Imeangaza dunia nzima, na sasa itafungua milango kwa watu kujifunza mengi kuhusu Afrika, kupitia muziki wa Afrobeats," anasema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live