Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akon: Kuwa na wake wengi ni bora

Akon Wake Wengi Akon

Mon, 17 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nguli wa muziki aliyewahi kufanya vyema nchini Marekani Aliaune Damala Badara Akon Thiam maarufu kama 'Akon' amesema kuoa wake wengi kwake ni chaguo bora kabisa.

Akon Kwenye Mahojiano Na Big Boy Amesema Kwamba Kuwa Na Wake Wengi Ndio Chaguo Bora.

Katika sehemu ya mahijiano yake Akon anasema;

Big Boy: Mimi ninaye mmoja tu inamaana wewe umenizidi mimi ?

Akon: Iko hivyo bila shaka, Na maisha yako Ni magumu kwa sababu unatazamia kitu kimoja tu muda wote. Ni bora kuwa Na wengi.

Big Boy: Ebu nielezee maana mimi nina mmoja tu, Labda naweza kuongeza wengine.

Akon: Sawa...ngoja nieleze vizuri ili wasije wakanitafsiri tofauti kwa mfano: una suruali 4 tofauti zenye rangi tofauti, kila siku una uhakika wa kuvaa bila kurudia na ndiyo maisha yako yanaonekana bora na mepesi, Lakini ukiwa nayo moja tu halafu nyekundu utajikuta unasema dah nitarudia kweli hii hii Kesho !!? Kwahiyo Huwezi Ukawa unavaa vazi moja kila siku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live