Mtu mmoja, mwenye kipaji cha kuigiza sauti za watu maarufu raia wa Italia amekiri kuiba zaidi ya miswada 1,000 ya vitabu ambavyo haviijachapishwa, mingi ikiwa imeandaliwa na waandishi mashuhuri.
Filippo Bernardini alikuwa akiwaiga watu mashuhuri kwenye tasnia ya uchapishaji ili kuwahadaa watu ili wakabidhi kazi zao kwake.
Kwa ufupi alikuwa akijifanya kama mhariri, ama mchapishaji, ama muandaaji kutoka kampuni fulani ambayo inaaminika, kwa sauti yake na matendo yake wengi walifikiri ni mtu sahihi na kutoa kazi zao kwako, kumbe alikuwa akiiwaiga
Alitumia ujuzi wake wa ndani wa tasnia, akiwa ameajiriwa na kampuni kubwa ya uchapishaji Simon & Schuster huko London.
Bernardini, 30, amekutwa na hatia ya kufanya matendo hayo ya kulaghai huko New York, lakini nia yake haijawahi kuwa wazi.
Baada ya kupata miswada hiyo, haikuvuja kwenye mtandao, wala hakudai madai yoyote ya fidia.
Kuhukumiwa kwa Bernardini, ambaye alikamatwa na FBI Januari mwaka jana, inaonekana kuelezea fumbo ambalo limesumbua ulimwengu wa fasihi kwa miaka, huku Margaret Atwood, Ian McEwan na Sally Rooney wakiwa miongoni mwa waandishi wanaolengwa.
Waendesha mashtaka walisema alisajili zaidi ya akaunti 160 bandia vya mtandao kuanzia 2016, kutekeleza azma yake.