Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Akimbia umbali wa kilomita 160 kumuona mchumba

Akimbiaaaa Akimbia umbali wa kilomita 160 kumuona mchumba

Wed, 11 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume mmoja huko San Diego aliyefahamika kwa jina la Aron Greene (26) ametengeneza rekodi ya kipekee na hii ni baada ya kukimbia takribani Miles 100 ambayo ni sawa na kilomita 160 kwa ajili ya kwenda kumuona mchumba wake.

Unaposema kilomita 160 kwa wale ambao wanasafiri mara kwa mara watakuwa mashuhuda juu ya umbali huu, lakini kwa faida ya wengi huu ni umbali kutoka Dar es salaam mpaka Mikese ambayo ni Morogoro.

''Nilikuwa nimesimama kwenye makutano ya barabara kubwa nikasema nadhani naweza kufika kwake kwa kukimbia tu'' alisema Aron Greene ambaye alikuwa anatoka San Diego kuelekea Los Angel alipo mpenzi wake, jambo ambalo lilimchukua takribani saa 32 yaani siku moja na saa 8.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live