Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Ajiua nakuagiza mazishi yake yafanyike Februari 14

MAITI YAPOTEA Ajiua nakuagiza mazishi yake yafanyike Februari 14

Thu, 8 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwalimu mmoja wa kiume katika kaunti ya Embu amewashangaza wengi baada ya kujitoa uhai kisa kukataliwa na mpenzi wake wa zamani huku akiacha barua ya jinsi atakavyozikwa.

Kwa mujibu wa maelezo yake kwenye Facebook, Dennis Mwaniki maarufu kama Mkono, mwenye umri wa miaka 32 alianza kwa kuwaalika marafiki zake kwa shughuli yake kuu itakayofanyika siku ya wapendanao, Februari 14.

Bila kujua, kumbe alikuwa anatoa mwaliko kwa watu kuhudhuria mazishi yake kwani alikuwa tayari ameratibu kujitoa uhai kisa kukataliwa na aliyekuwa mpenzi wake.

Kamanda wa Polisi wa Kaunti ndogo ya Mbeere Kaskazini Eric Yego alisema MCA wa Nthawa Sammy Tito alitoa ripoti katika Kituo cha Polisi cha Siakago kwamba mwanamume mmoja hakuwa akipokea simu kutoka kwa marafiki na familia na alikuwa amejifungia ndani ya nyumba yake katika kijiji cha Nthangariri.

Yego alisema polisi walivunja mlango ili kuingia ndani ya nyumba hiyo na walimpata Mwaniki akiwa amekufa juu ya kitanda chake bila majeraha yoyote ya mwili isipokuwa damu na vitu vyeupe vinavyotoka puani.

Barua ya kujitoa muhanga inayoaminika kuandikwa na Mwaniki ilipatikana ndani ya nyumba hiyo. Katika maelezo hayo, marehemu alieleza kwa nini aliamua kukatisha maisha yake.

Aliagiza kwamba mazishi yake yafanyike Februari 14. Mwaniki alionyesha katika noti hiyo nambari ya simu ya mwanamke ambaye alimwagiza asome ujumbe wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live