Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Agizo la Rais JPM kuhamisha Cosota lakamilika

Cosota+pic COSOTA

Thu, 16 Jul 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

WIZARA ya Viwanda na Biashara imeikabidhi rasmi Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Chama cha Haki Miliki (Cosota).

Hatua hiyo inakuja ikiwa siku nne zipite tangu Rais John Magufuli kuahidi kufanya hivyo, aliwahidi wasanii kufanya hivyo katika hafla ya chakula cha mchana aliyowaandalia wajumbe wa mkutano mkuu CCM iliyofanyika Chamwino Dodoma.

Tukio hilo la makabidhiano limefanyika leo Jumatano jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Prefesa Riziki Shemdoe na Katibu wa Wizara ya Viwanda, Hassan Abbas na kushuhudiwa na wasanii wa tasnia mbalimbali ikiwemo filamu, muziki, sanaa za maonyesho na ufundi.

Akizungumza katika hafla hivyo, Katibu wa Viwanda aliwataka Cosota ikaendeleze mipango iliyowekwa  kwa kuwa kazi wanazoenda kuzifanya ni zilezile jambo litakalosaidia wasanii kufaidika na kazi zao.

Naye Katibu wa Wizara ya Habari, Dk Hassan Abbas, amesema uamuzi wa kuihamisha taasisi hiyo, yalikuwa magumu lakini Rais Magufuli amefanya maamuzi magumu.

Dk Abbas pia amesema ndani ya saa 24 atakutana na Bodi ya Cosota kujua mikakati yao ya namna gani ya kumfanya msanii kuwa  tajiri na kuhusu malimbikizo ya mirabaha yao ambayo wamekuwa wamekilalamikia.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz