Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika Mashariki na Magharibi tunaongoza kwa tamthilia zenye ubora – Steve Nyerere

4655 19623701 2028678487365452 1953297808496787456 N E1520860509199 TZW

Mon, 12 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Msanii wa filamu Bongo, Steve Nyerere amesema tasnia hiyo kwa sasa inaongoza Afrika Mashariki na Magharibi kwa kutoa tamthilia zenye ubora.



Muigizaji huyo ameiambia Clouds Fm kuwa mafanikio hayo yamefikiwa baada ya wasanii kugundua sehemu waliyojikwaa na kuamua kuinuka na kuanza upya.

“Tumesimama sasa katika Afrika Mashariki na Magharibi yote tunaongoza kwa kuonyesha tamthilia zenye ubora, inaonyesha ni kwa kiasi gani Tanzania kuna vipaji,” amesema.

Ameongeza kuwa kilichobaki kwa sasa ni wasanii kuongeza thamani ya kazi zao na kujithamini na sio kuwa kawaida kwenye kila jambo ambalo wanafanya.

Chanzo: bongo5.com