Mkongwe wa muziki wa Hip Hop, Selemani Nyandindi maarufu kama Afande Sele amesema kuwa hakualikwa kwenye shughuli ya uzinduzi wa Taasisi ya Profesa Jay iliyofanyika weekend iliyopita katika Ukumbi wa Mlimani City.
Mshindi huyo wa Tuzo ya Mfalme wa Rhymes mwaka 2004, amesema kuwa shughuli ya Profesa Jay iliandaliwa na watu maalum na hakuiandaa mhusika mwenyewe ndiyo maana baadhi ya wasanii hawakupata mwaliko wa kuhudhuria kumuunga mkono mkongwe huyo wa Bongo Fleva.
“Nimeona kuna mjadala unaendelea, unahusisha tukio kubwa na jema la uzinduzi wa taasisi ya ndugu yetu Profesa Jay pale Mlimani City, tukio maalum kabisa lile.
“Kuna watu naona wanajaribu kutumia tukio hili kutafuta kick au ku-trend mjini, wanawalaumu wasanii ambao hawakuwepo na kuwapongeza wasanii waliokuwepo. Wanashindwa kujua kwamba hili ni tukio maalum ambalo kuna waandaaji wameliandaa na huwezi kwenda pale kama sokoni au msalani, lazima uwe na mwaliko ndipo uweze kwenda.
“Mwingine anasema hadi Ferouz ndugu yake hajaenda, siyo Ferouz tu, mimi mwenyewe ndugu yake Afande Sele sijaenda. Mimi na Jay tumepita chochoro zote, kuanziaalbamu ya Machozi, jasho na Damu.
“Hata wakati akigombe ubunge, ukienda Mikumi watakwambia, tulikwenda Kijiji kwa Kijiji wakati anaenda kujitambulisha kwa mara ya kwanza kabisa. Tulipiga kazi usiku na mchana na ndugu yangu mpaa akaja kuwa mbunge baadaye.
“Hata alipoanzisha Kampeni ya “Nishike Mkono”, mimi nilikuwa naye bega kwa bega. Hata kwenye mahojiano ndugu yangu siyo mchono wa fadhira, ananitaja nilikuwa na akina Afande Sele, Darassa, Stamina lakini kwa nini na mimi juzi hujaniona?
“Ni kwa sababu lile ni tukio maalum lina mwaliko maalum na walioandaa ndiyo wamepanga nani aje nani asije. Lakini kama angeandaa ndugu yetu Jay kwa asilimia 100, bila shaka watu wake wote wa karibu ungewaona,” amesema Afande Sele.
Profesa Jay ameanzisha taasisi hiyo kwa ajili ya kuchangisha fedha kusaidia watu mbalimbali wenye matatizo ya figo lakini wamekuwa wakipoteza maisha kwa kushindwa kupata huduma kutokana na kukosa pesa za matibabu.