Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afande Sele: Mandonga alikuwa baunsa wangu, anapenda kula sana

MANDONGA MTU KAZI Afande Sele na Mandonga

Tue, 2 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii nguli wa rap, Afande Sele amemzungumzia bondia anayetrend kwa sasa nchini Karim Mandonga kwa kusema kwamba anapenda sana kula chips na kufanya mazoezi na kwamba ngumi ni kazi yake ya miaka mingi.

Afande amefunguka hayo kufuatia bondia huyo kupigwa na bondia Shabani Kaoneka kwa TKO jambo ambalo wengi hawakulitarajia kutokana na majigambo ya bondia huyo kutoka viunga vya Msamvu Morogoro.

“Mandonga ndio jina maarufu sana lakini mimi namfahamu kama Karim, ni mdogo wangu na rafiki yangu wa karibu sana. Namfahamu kama dawa maji na yeye akanifahamu kama King Sele, ni familia ya Watu Pori, Gheto Boys.

“Namfahamu kama mpiga kazi wa pale stendi Msamvu (Morogoro), ni mpambanaji. Kazi ya ngumi hajaanza leo, watu wa Morogoro wanamjua tangu kitambo kwamba ni mtu wa boxing, Mtu Kazi. Kwenye pambano lake anaondoka na kijiji pale Msamvu.

Tangu enzi za akina Francis Cheka, Mandonga alikuwa anapenda boxing. Kuna wakati nilikuwa nikisafiri kwenye shows zangu naenda naye kama baunsa wangu. Mkifika pengina mkachukua gesti yeye anaingia kufanya mazoezi kwenye chumba chake, akitoka mwili wote una joto, ukiingia chumbani kimechemka, yaani kapasha mpaka chumba kimekuwa cha moto.

Karim sio mtu wa mitungi sana, anapenda misosi, mkifika sehemu labda ukaagiza bia moja yeye anaagiza chipsi yai moja, mkiagiza bia ya pili na yeye anaagiza chipsi ya pili, yaani ukimaliza idadi yako nay eye anakuwa amekula chupsi yai idadi ya bia ulizokunywa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live