Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adidas yasema inapanga kuuza viatu vilivyosalia vya Yeezy

Adidas Yasema Inapanga Kuuza Viatu Vilivyosalia Vya Yeezy Adidas yasema inapanga kuuza viatu vilivyosalia vya Yeezy

Thu, 1 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Adidas inasema inapanga kuuza viatu vya Yeezy vilivyosalia kutoka kwa ushirikiano wake uliofeli na Kanye West hata kama ni kwa gharama fulani.

Kampuni hiyo ilikata uhusiano na rapper huyo na mbunifu wa mitindo, ambaye pia anajulikana kama Ye, mnamo 2022 baada ya kutoa maoni kadhaa ya chuki kwenye mitandao ya kijamii.

Lakini mahitaji ya viatu vya Yeezy hayajaisha, kwani vinasalia kuwa maarufu sana katika soko la uuzaji.

Hili linawadia baada ya mabadiliko ya sarafu kusababisha hasara ya €1bn ($1.08bn; £850m).

Mapato ya kampuni hiyo kubwa ya nguo za michezo nchini Ujerumani yaliathiriwa mwaka jana kwa kusitishwa kwa biashara ya Yeezy huku ikipunguza bei kwa wauzaji wa jumla ili kupunguza akiba ya bidhaa hiyo, Adidas ilisema katika taarifa yake.

Licha ya kukabiliwa na misukosuko mikubwa, Adidas ilichapisha faida ya uendeshaji ya €268m mnamo 2023 na ilisema inatarajia karibu mara mbili ya kiwango hicho mwaka huu.

Bw Gulden aliletwa kutoka kampuni pinzani ya nguo za michezo ya Puma mwanzoni mwa 2023 ili kuendesha mabadiliko ya Adidas baada ya kukatisha uhusiano na brand ya Yeezy ambako kuliwaacha na viatu ambavyo havijauzwa vya thamani ya takriban €1.2bn.

Ingawa kampuni iliuza baadhi ya viatu vyake vya Yeezy mwaka jana, mauzo ya jumla kutoka kwa ushirikiano huo yalikuwa karibu €450m chini kuliko 2022.

Chanzo: Bbc