Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adele aweka rekodi ndani ya saa 24

Adele 11 Adele aweka rekodi ndani ya saa 24

Sat, 16 Oct 2021 Chanzo: eatv.tv

Nyota wa muziki kutoka Uingereza Adele ametumia saa 24 tu kuvunja rekodi ya wimbo wake “Hello” wa mwaka 2015 huko YouTube na Spotify baada ya ‘Easy On Me’ kuwa gumzo kwenye kila platform za muziki Duniani kote.

Spotify wamethibitisha kuwa wimbo huo mpya kutoka kwenye albamu yake ya nne ‘30’ umeweka rekodi ya kusikilizwa zaidi katika mtandao huo licha ya kutokuweka wazi idadi ya streams, na awali rekodi hiyo ilikuwa inashikiliwa na BTS kupitia ‘Butter’ baada ya kufikisha streams Milioni 11.04.

Pia ‘Easy On Me’ huko YouTube umefikisha watazamaji zaidi ya Milioni 49 ukilinganisha na “Hello” ambao ulipata watazamaji zaidi ya Milioni 27 ndani ya siku moja.

Chanzo: eatv.tv