Waimbaji wa Uingereza Adele na Ed Sheeran wameripotiwa kuupiga chini mualiko wa kutumbuiza kwenye hafla ya baada ya tukio la kutawazwa Mfalme Charles III, Mei 7 mwaka huu.
Kwa mujibu wa muaandaji wa tukio hilo, King Charles ndiye alipendekeza majina hayo mawili kuwa sehemu ya juu kwenye orodha ya washereheshaji.
Ed Sheeran ameripotiwa kuupiga chini mwaliko huo kufuatia kubana kwa ratiba yake ambapo ameeleza kwamba atakuwa akitumbuiza mjini Texas, siku kabla ya tukio la kutawazwa mfalme hivyo inakuwa kuweza kusogeza mbele.
Kwa upande wa Adele, hakuna sababu yoyote ambayo imetolewa na ratiba yake inaonesha hatakuwa na onesho lolote la wazi baada ya Machi 25.