Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adam Mchomvu amnyooshea mikono Rayvanny

Rayvanny Basi.jfif Adam Mchomvu amnyooshea mikono Rayvanny

Tue, 27 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtangazaji wa Radio wa muda mrefu na msanii wa Hip Hop nchini, Adam Mchomvu amedai Rayvanny ni msanii anayebadili game ya muziki nchini kwa kile anacho kifanya kwenye shows zake za Fiesta, hasa alicho kifanya Tabora jumamosi iliyopita ya September 24, akifananisha ubunifu huo na kile kinacho fanywa kwenye shows kubwa kama Superbowl Halftime Shows

Kiukweli Rayvanny amefanya kitu kikubwa sana, kuna watu wanabeza na kuona anapoteza hela kubwa kwenye maandalizi ya shows zake kuliko anacho ingiza, ila wanasahau, Kuijenga Brand yako pesa inatoka kuzidi unacho ingiza, ndicho anacho kifanya Rayvanny kwasasa. Lakini pia, hatujui anaingiza kiasi gani, Makubaliano yanabaki kuwa siri baina ya pande mbili.

Tunahitaji Creativities nyingi kwenye shows kama hizi, zaidi ya kuhitaji audience iinue mikono juu na kuipeleka kushoto na kulia. Imani yangu ni kuwa yale majukwa ya MTV Emas, Dubai expo ni Experience kubwa sana aliyopata Rayvanny hadi kuyafanya haya hapa Bongo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live