Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adam Juma: P Funk aheshimiwe, vinginevyo dunia itakua nyeusi

Adam Juma P Funk Adam Juma: P Funk aheshimiwe, vinginevyo dunia itakua nyeusi

Wed, 20 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muongozaji mkongwe wa video nchini, Adam Juma ameibuka na kumtetea producer mkongwe wa muziki nchini P Funk Majani kufuatia bifu lake na Lebo ya WCB akisema heshima ya procuder huyo inatakiwa pale pale.

Adam Juma amesema hayo kufuatia kauli ya P Funk kuwa WCB inawakandamiza na kuwanyonya wasanii wake jambo ambalo liliibua mijadala huku WCB wakimtupia madongo mkongwe huyo.

Kauli ya Majani ilipokelewa tofauti kwa upande wa WCB na kupelekea kuwepo kwa majibizano mtandaoni yaliyoanzishwa na Baba Levo kisha baadae meneja wa msanii Diamond Platnumz, Sallam SK, babu Tale na Mkubwa Fella wote wakimjibu Majani.

Adam amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram; "Huyu mzee tuseme yote heshima yake kwenye tasnia yetu ibaki pale pale vinginevyo dunia itakua nyeusi sana. Hatuna nguvu ila tupo wengi. Vita ya mawe kwenye kokoto," amesema Adam Juma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live