Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Achana na gari, Harmonize kamnunulia Kajala nyumba

Harmonizee Pic Data Achana na gari, Harmonize kamnunulia Kajala nyumba

Mon, 1 Mar 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Nasra AbdallahMore by this Author ‘Couple’ kati ya msanii wa filamu, Kajala Masanja na mkali wa ngoma ya Uno, Harmonize inazidi kunoga na sasa ni mwendo wa mazawadi kila uchwao.

Wawili hao walianika rasmi mahusiano yao Februari 14, mwaka huu, kwenye sikukuu ya Wapendanao na kuibua gumzo huko mitandoni na kwa wafuatiliaji wa masuala ya burudani kwa ujumla.

Pia katika hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na benki ya CRDB hivi karibuni ambapo Harmonize ni balozi wao, alimtambalisha Kajala kama mke wake kwa kumuita jukwaani ili watu wamuone.

Juzi kati wapendano hao tena wakaja na jipya baada ya kusambaa kwa picha zikimuonyesha Harmonize akimkabidhi funguo za gari Kajala ambaye wakati huo alikuwa mazoezini.

Gari hiyo aina ya Crown Athelete inaelezwa kuwa thamani yake ni kati ya Sh12 milioni hadi Sh13 milioni.

Hata hivyo, mtu wa karibu na msani huyo, alisema ukiachana na gari, Kajala tayari amenunuliwa mjengo eneo la uwekezaji wa nyumba za Himidu City zilizopo maeneo ya Kigamboni, Dar es Salaam ambapo nyumba zake zinaelezwa huuzwa kati ya Sh114 milioni hadi Sh260 milioni.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz