Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Abu Salami: Davido hana hela, anaigiza

Abu Salami: Davido Hana Hela, Anaigiza Abu Salami: Davido hana hela, anaigiza

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mpigapicha na mfanyabiashara, Abu Salami amedai kuwa msanii kutoka nchini Nigeria Davido hana pesa bali msanii huyo anaishi maisha ya uongo.

Hii inakuja baada ya mpigapicha huyo kutoelewana na Davido katika simu kuhusiana na deni la N218 Milion kwa ajili ya mradi wa watoto ambapo amedai kuwa msanii Burna Boy na Rema ni matajiri kushinda Davido.

Hii ni mara ya pili mwaka huu kwa Davido kushutumiwa kwa kushindwa kutimiza majukumu ya kimkataba, hapo awali, Rais wa zamani wa Shirikisho la ‘Soka’ la Nigeria, Amaju Pinnick, alimuita hadharani Davido kwa kutoheshimu mkataba wake nao.

Davido ambaye kwasasa anatamba na album yake ya ‘Timeless’ huku wimbo ambao umeibeba albamu hiyo ukiwa ni ‘Unavailable’.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live