Mbunge wa Jimbo la Morogoro mjini Abdulazizi Abood amemtembelea msanii wa bongo fleva Selemani Msindi maarufu kwa jina la Afande Sele.
Abood amemtembelea Afande Sele ili kumjula hali msanii huyo baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo siku chache zilizopita na sasa ameruhusiwa.
Mbunge Abood amesema yupo tayari kushirikiana na wasanii kwani ni kundi muhimu katika kusaidiana kuleta maendeleo.
Amesema jukumu la viongozi kuwajali wananchi wote hivyo yeye kama kiongozi anawajibu wa kuwatembelea watu wote bila kubagua.
Kwa upande wake Afande Sele amemshukuru Mbunge huyo kwa kumtembelea na kumpa moyo katika kipindi hiki kigumu anachopitia.