Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Abiria wa ndege waachwa kisa uzito

Abiria Ms Abiria wa ndege waachwa kisa uzito

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Ndege la Japan, hivi majuzi lililazimika kuwakataa baadhi ya abiria kwenye Ndege zao mbili kutokana na uzito.

Abiria hao ni wachezaji wa Mieleka ya Sumo, mchezo wenye asili ya Japan. Tukio hilo lilitokea wakati mamia ya wachezaji wakielekea kwenye Mashindano katika Kisiwa cha Amami Oshima nchini humo.

Japan Airlines imesema hali hiyo hutokea kwa nadra sana. Shirika lililazimika kufanya hivyo kwani uzito wa jumla wa abiria ungeliweza kuizidi nguvu Ndege.

Baada ya kufanya hesabu za jumla ya uzito, Shirika hilo lililazimika kuandaa Ndege ya ziada ili kuwabeba wanaume hao kwani kila mmoja alikuwa na uzito wa takribani kilo 120, wakati uzito wa kawaida wa abiria wao wa kawaida huwa na wastani wa kilo 70.

Wanamieleka hao walitarajia wangesafirishwa kwa Ndege kubwa hata hivyo maafisa wa Shirika hilo walisema uwanja wa Ndege wa Kisiwa hiko ni mdogo mno kuweza kupokea ndege kubwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live