Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Abigail Chams: Nilienda Tanga kujifunza kupika ugali

Abigail Chams Abigail Chams: Nilienda Tanga kujifunza kupika ugali

Fri, 8 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya mwanamuziki wa #bongofleva nchini Abigail Chams ku-share video akiwa anasonga ugali, ameweka wazi kuwa alienda mkoani Tanga kwa ajili ya kujifunza kupika chakula hicho.

Abigail ameyaseama hayo kwenye mahojiano yake na vyombo vya habari siku ya jana katika uzinduzi wa Samia Queens ambapo alieleza kuwa yeye ni mtu ambaye akipewa challenge lazima aifanye, watu walimzodoa sana kuwa hawezi kusoga ugali ndipo akaamua kwenda kujifunza.

Aidha kupitia mahojiano yake hayo amedai kuwa alienda Mkoani Tanga kwa ajili ya kujifunza kupika chakula hicho na haikuchukua muda sana wa yeye kuelewa jinsi ya kupika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live