Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Abdulrazack: Diva ameshika mimba tatu

Diva 2 Mumee.png Abdulrazack na Diva

Wed, 31 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtangazaji wa kipindi cha Lavidavi cha Wasafi FM, Diva The Bauswe na mumewe Abdulrazack wameamua kufunguka mengi kuhusu maisha yao huku mumewe huyo akidai kuwa Diva hana tatizo la uzazi.

Katika kipindi hicho cha Mapito Mtangazaji Alimuuliza swali Mume wa Diva ambaye aliongozana naye katika kipindi hicho, Abdulrazack kuhusu kuwa na mtoto na historia yake ya kushindwa kupata mtoto katika nyakati tofauti.

“Nilichogundua mimi kwa miezi saba niliyokua naye ni kwamba Diva hana shida ya uzazi na mpaka sasa ameshashika mimba mara tatu isipokua mfuko wake wa uzazi upo dhaifu,” alisema mume wake Abdulrazack.

Aliendelea kwa kusema kuwa ili aweze kupata mimba ambayo itamfanya apate mtoto itabidi apate muda wa kupumzika kwa miezi mitatu ambapo kitu hicho ni kigumu kutokana na kazi anazozifanya alimalizia Abdulrazak amabaye ni Mume wa ndoa wa Diva.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live