Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Abby Chams amchamba TID kisa kusonga ugali

TID  (17) Abby Chams.jpeg TID na Abby Chams

Wed, 3 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Kizazi kipya Cha Bongofleva AbbyChams ameonesha kutopendezewa na jambo alilolisema TID kuwa hajui kupika Ugali.

Hayo ameyasema kufuatia kauli ya TID aliyoizungumza hivi karibuni yakusema kuwa ameshangazwa na mrembo huyo kusema hajui kupika Ugali jambo ambalo sio Utamaduni wa Mtanzania.

AbbyChams amemjibu TID kwenye moja ya Mahojiano aliyofanya na Vido Vidox amesema kwamba

"Kwanza nilikuwa sijui TID ni nani nikaona kuna mbabu ana kipara ananizungumzia kwenye social media (mitandao ya kijamii) kwamba sijui kusonga ugali mi nikaona nisiseme chochote kwa sababu mimi nimelelewa kuheshimu Watu Wazima halafu nikimuangalia anaonekana kama kama sio Baba yangu basi nadhani atakuwa mkubwa zaidi ya Baba yangu.

"Lakini nilijufunza kitu kwamba Mabinti wengi wanashindwa kuendelea kwa sababu mitazamo ya watu wengi wanafikiria Msichana lazima ujue kusonga Ugali ndio unakuwa Mwanamke jambo ambalo sio kweli

"Na nimegundua kitu kingine Wababa Watu wazima badala ya kutumia Mitandao ya Kijamii kitu-empower sisi Mabinti zao ili tujifunze kutoka kwao Wanatumia Mitandao kukisema vibaya kizazi kipya Cha Muziki.

"Kwa hiyo Mimi ninamuombea tu awe na hekima kulingana na umri wake. Mimi nyumbani kwetu huwaga hatuli sana ugali kwahiyo sikuwahi kujifunza kupika Ugali," amesema AbbyChams.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live