Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Abby Chams: Marioo nimefutilia mbali

Marioo Abby Srd Abby Chams: Marioo nimefutilia mbali

Sun, 1 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva, Abigail Chamangwana 'Abby Chams' amesema kuwa msanii wa Bongo Fleva, Omary Ally Mwanga maarufu kama Marioo hana washauri wazuri hasa kwenye kuchagua kipi cha kuzungumza hadharani na kipi si cha kuzungumza.

Abby Chams amesema hayo wakati akihojiwa na mtangazaji Alfred Bundala wa SNS kufuatia wawili hao kupishana mitandao kisa kikidaiwa kuwa Marioo kufuta verse ya Abby kwenye ngoma yake ya Love Song.

“Sijaongea na Marioo kwa muda mrefu, mimi ni mtu ambaye sijalelewa kujibizana au kuzungumza kwenye mitandao ya kijamii, si na muda wala nguvu ya kufanya hivyo. Ninajiheshimu kuanza kuingia mtandaoni na kumtukana mtu ningekuwa mjinga.

“Abbah ndiye mtu ambaye nina ukaribu naye na bado tunafanya kazi pamoja ila Marioo ni kama hayuko kwenye maisha yangu. Nimefutilia mbali. Mimi kitu chochote kikitokea namuachia mungu, yeye mwenyewe atajuana na Mungu huko mbeleni.

“Kum-unfollow mtu lazima upate muda w akum-search jina lake, aisee mimi muda sina lakini namba ipo kwenye simu bado sijaifuta,” amesema Abby Chams.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live