Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Abby Chams: Marioo hana washauri

Abby Chams Marioo.png Abby Chams: Marioo hana washauri

Fri, 29 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva, Abigail Chamangwana 'Abby Chams' amesema kuwa msanii wa Bongo Fleva, Omary Ally Mwanga maarufu kama Marioo hana washauri wazuri hasa kwenye kuchagua kipi cha kuzungumza hadharani na kipi si cha kuzungumza.

Abby Chams amesema hayo wakati akihojiwa na mtangazaji Alfred Bundala wa SNS kufuatia wawili hao kupishana mitandao kisa kikidaiwa kuwa Marioo kufuta verse ya Abby kwenye ngoma yake ya Love Song.

“Kulikuwa na hii ngoma ya Marioo, akanisikilizisha, ni nyimbo ambayo ni nzuri tukakubaliana tukaenda studio tukaifanya, nilirekodi verse yangu ya kwanza, na yeye akarekodi ya kwake ya pili lakini hakumalizia. Nilirudi nyumbani kama saa 12 alfajiri kwa sababu ilikuwa session ndefu, sijui kilichotokea.

“Kuna siku nikamcheki kumuuliza hii ngoma ni kali tutaimalizia lini, akasema atanicheki aniambie lini tutaimalizia. Siku moja nikaamka nikakuta ngoma imeshatoka, nilishangaa tu ikabidi niruhusu.

“Sio kweli kwamba nilikuwa siupendi ule wimbo, kama alinisikilizisha, nikaenda studio na tukaifanya kwa nini niseme sijaipenda, ule ulikuwa niliona kabisa ni wimbo mzuri. Sijui kwa nini alisema hivyo, labda kwa sababu ya kujitetea.

“Nilishtuka kusikia maneno aliyosema Marioo kwamba sina shukrani, yule ameshakuwa mtu mzima anajua kwamba akisema jambo kwenye public madhara yake ni makubwa na haitakiwi kisheria. Nadhani hana washauri wazuri," amesema Abby Chams.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live