Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aaron Taylor-Johnson ndiye James Bond mpya

Aaron Taylor Johnson Vs James Bond Aaron Taylor-Johnson na James Bond.

Thu, 21 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwigizaji wa filamu, Aaron Taylor-Johnson anatarajiwa kuchukua nafasi ya Daniel Craig kuwa James Bond wa saba, jasusi wa upepelezi anayetambulika kwa namba 007 kwenye shirika la kijasusi la MI6 la Uingereza.

Jina la Aaron Taylor-Johnson ndilo limebamba kwenye vyombo vya habari vya Uingereza, tofauti na majina mengine likiwamo la Mwingereza mweusi, Damson Idris (32), aliyeigiza kwenye filamu za Snowfall na Black Mirror. Tangu filamu za James Bond zianze zaidi ya miaka 50 iliyopita hakujawahi kuwa na James Bond mweusi.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uingereza, Taylor-Johnson atasaini mkataba wiki hii wa kuanza jukumu la James Bond mpya, akiigiza kama jasusi mwenye namba ya utambulisho 007.

Taylor-Johnson ambaye ni nyota wa filamu za Kick-Ass, ametajwa ndiye anayeweza kuwa James Bond wa saba, baada ya Craig ambaye amekuwa mpelelezi maarufu kwenye filamu hizo kwa miaka mingi akitumia namba ya utambulisho ya 007.

Craig (56) ameacha jukumu la kucheza kama James Bond mwaka 2021 baada ya kuigiza filamu tano kwa zaidi ya miaka 16 na filamu yake ya mwisho ni ‘No Time To Die’.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live