Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Aanguka na kufa wakati akisakata rhumba kwenye 'birthday'

Kufabirthday (1) Aanguka na kufa wakati akisakata rhumba kwenye 'birthday'

Mon, 8 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati wa huzuni ulishuhudiwa katika hafla ya mwanamume mmoja mwenye umri wa makamo ambaye alikuwa anasherehekea kwa mbwembwe siku yake ya kuzaliwa.

Katika tukio hilo la furaha ambalo liigeuka na kuwa la huzuni, mwanamume huyo akiwa amevalia suti nyeusi alianguka sakafuni na kufariki wakati anacheza densi kwa furaha kufikisha mwaka mwingine.

Mwanamume wa siku ya kuzaliwa kwenye video alionekana kwenye jukwaa la katikati akicheza huku na huku waliohudhuria wakitazama na huo ulikuwa mwanzo tu.

Alipoendelea kucheza siku ya kuzaliwa kwake, mwanamume huyo aliteleza na kuanguka ghafla na kwa ugani Zaidi alijikuta sakafuni.

Kwa wakati huu, kila mtu kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa alihisi mwanamume huyo anajaribu kuigiza hadi pale walipopigwa na butwaa ya ukweli kwamba mwili wake hungeweza kusojnga tena.

Hapo ndipo Mwanaume mmoja alijongea karibu naye kama njia ya kumchunguza na hii iliwafanya wanaume wengine kuthibitisha kinachoendelea hadi kutangazwa kuwa amekufa.

Sauti ya mwanamke aliyekuwa nyuma ilisikika ikisema "Subiri, hivi huu ni ukweli ama maigizo jamani? ni kweli?" kwani wengi wa waliohudhuria sherehe ya siku ya kuzaliwa hawakuamini macho yao tena.

Wengine wakijibu video hiyo walidai kuwa mtu huyo wa kuzaliwa alikuwa na kifafa kabla ya kufa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live