Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AY, The Pathbreaker of Bongo Flava (Part II)

AY 6 AY.

Wed, 17 Apr 2024 Chanzo: Luqman Maloto

Raha Kamili” ilikuwa jina la albamu ya kwanza ya AY. Ya pili “Hisia Zangu". Kabla ya kuziendea hisia za AY, kuna mambo ni mortal sin kuyaruka kuhusu AY, Swahili Rap na Bongo Flava kwa jumla.

Tuanze na “Njoo Kati” ya Zay B feat AY na Complex. Umewahi kujiuliza sauti ya AY ingekosekana ule mkwaju ungekuwaje? Halafu, kuna verse, kisha ipo mipito ya ki-El-Chapo kutoka kwa AY. Hiyo ni tafsiri kwenye dude “Umuhimu”, kazi ya Vivi.

Okay, undava wa AY unaanzia kwenye hook. Ameumiza si kitoto. Kisha, verse ya pili, mitambao ya AY ndani ya mistari 16. Minato ya kibingwa kwenye mdundo. AY ndiye kila kitu kwenye wimbo “Umuhimu”. Vivi akatambulika kwa urahisi. AY made it simple.

Then we have “Mawazo” ya Lady Jaydee. Kitu cha kujadili, AY siyo flat rapper. Anajua kucheza na mizunguko ya beats kwa namna ambavyo mpenda muziki utamwona special jinsi anavyohama bar-to-bar. Ndivyo AY amepita ki-Masta katika verse ya tatu ya “Mawazo” by Jide.

Tuiweke mezani “Hisia Zangu”, AY kwa maono makubwa, aliingiza sound mpya kwenye Swahili Rap. Kituo Kampala, Uganda with Maurice Kirya, kazi tamu sana “Binadamu”.

Kuhusu topic, AY alikuwa kwenye kampeni ya kushughulika na walimwengu, alioanza nao katika “Machoni Kama Watu” feat Jide. “Binadamu” ni feather in the cup of AY. Wimbo uliupeleka muziki wa Tanzania katika level ya juu kabisa. Hii ndiyo sababu AY ni exceptional.

Albamu ya kwanza “Raha Kamili” ilikuwa kazi ya kitaifa. Alishirikisha artists kutoka Nyerereland peke yake. “Hisia Zangu” alifungua mipaka ya Afrika Mashariki, kutoka Maurice Kirya Uganda hadi Prezzo Kenya kwenye “Nipe Nikupe”. Halafu upo ule mdude “Yule” ambao warembo club walipatwa uchizi kila DJ alipoufungulia.

Ongeza “Yule Remix” with Deux Vultures wa Kenya. Kilichofuata, AY alianza kampeni ya kukusanya ladha kutoka Afrika, halafu akaifikia dunia. Ni sahihi mno kumwita AY “The Pathbreaker”. Amebisha hodi, akalazimisha, na akafanikiwa kufungua milango migumu.

Story ya AY haijafika mwisho. Na hivi ndivyo tunaiendea Aprili 26, 2024, AY atakapokuwa inducted kwenye jukwaa la Bongo Flava Honors. Tukio litakuwa Warehouse, Oysterbay. Ni siku isiyo na mfano.

Chanzo: Luqman Maloto