Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AY, The Blue-Chip of Bongo Fleva

Sugu Ay Mwana Fasf AY, The Blue-Chip of Bongo Fleva

Tue, 30 Apr 2024 Chanzo: Luqman Maloto

Wanasanaa bei mbaya huitwa blue-chip artists. Ambwene Allen Yessayah “AY” ni blue-chip artist. Neither graffiti za Banksy nor michoro ya Andy Warhol na Pablo Picasso, AY ni Bongo Flava.

AY ni mwanamuziki mkubwa Afrika. Angalau hili hatubishani. Bonus point ya ukubwa wa AY ni performance yake kwenye Bongo Flava Honors, Warehouse Arena, Oysterbay. April 26, 2024 ilikuwa AY day.

Kile ambacho AY alikionesha ndiyo kila kitu hadhira huhitaji kuona kwa mwanamuziki jukwaani. Haikuwa shoo ya watu 100 on stage kama Kanye West na All Day katika BRIT Awards 2015, AY peke yake with live band, alikonga kila nyoyo.

Delay kidogo ya kiufundi ilidhaniwa ingeharibu show. Haikuwa hivyo jombi. The main host, Sugu The Jongwe, alipopanda jukwaani atmosphere ilibadilika. Execution ya Kiburi, ilibadili mood from bad to good and even better.

Kama mchuano wa mavazi. Sugu na ice chain nyeupe juu ya shati nyeusi, miwani nyeusi, trouser na dundo Kenneth Cole white. AY ni all black. Sugu alipoachia jukwaa, AY alibadili mood ya audience from better to best.

Sauti, nishati, the chemistry na band, alivyodondosha hits dude kwa dude mbele ya crowd iliyokuwa hyped up, AY alifanya kila mtu atamani kuwa AY kwenye stage. Holy moly, inaachiwa Wapolo Remix, Joh Makini na Lord Eyez jukwaani.

Ikakitwa Hii Leo, Deputy Minister MwanaFA akapanda. Likafuata battle la Habari Ndiyo Hiyo. Tunasubiri jibu la Prof Janabi kama zile raha alizomimina AY Warehouse haziambukizi kisukari. The audience was super happy.

Ngosha Fid Q alikuwepo. Siyo tu alipanda jukwaani, alihakikisha heshima ya AY inafika mahali pake. Aliongoza msafara wenye mbwembwe nyingi kumsindikiza AY. Alipoona haelewi sauti, aliomba kuonana na sound engineer ili kuweka vitu sawa. It’s pure love from Fid Q to AY.

Nyomi la kutosha mashallah. Halafu players wote wakubwa kwenye industry walikuwepo. Wafanya uamuzi kwenye taasisi kubwa za kibiashara wali-show up for the love of AY, Bongo Flava Honors na tasnia.

Alichokifanya AY ndiyo huitwa "kumnyima hater fursa". Alifanya kila kitu kwa ubora mpaka wasaka fursa ya kukosoa wakabaki na zero. Vipo vya kusahau, siyo show ya AY Bongo Flava Honors.

Chanzo: Luqman Maloto