Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AT abadili rasmi jina lake

ALLI TOLU AT abadili rasmi jina lake

Wed, 26 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hatimaye msanii wa muziki wa Bongo Fleva kutoka Zanzibar Ally Tolu maarufu kama AT ametoa taarifa rasmi ya kutokulitumia tena jina la AT na sasa akitambulika kwa jina la BEY.

Bey @iamthebey ambaye hafanyi muziki wa mduara, kupitia ukurasa wake wa Instagram ameeleza kwamba moja ya sababu iliyomfanya akaachana na jina lake hilo la zamani ni kutokana na msanii mwingine nje ya Tanzania kutumia jina hilo.

"Hellow..!! Leo ni siku Special kwangu sababu najiona kama nimezaliwa upya kwenye game ya muziki.

Nilitangaza kuacha muziki wa mduara na leo rasmi natangaza kuachana na kutumia jina la AT kwa sababu nyingi, moja wapo ikiwa muingiliano wa jina langu na msanii mwingine ambae yupo nje ya mipaka ya Tanzania, ikiwa mipango yangu mikubwa ni kufika kimataifa nimeona nitumie fursa hii kujiandaa mapema.

Kwa sasa nitatambulika kama #BEY na sio AT, na nitakuwa kwenye mziki wa kisasa wa kibiashara zaidi na #YAYA ndio wimbo wangu wa kwanza kama #BEY ahsanteni.''

Chanzo: www.tanzaniaweb.live