Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

ASAP na Rihanna mahaba mazito

IMG 20220425 WA0012 613x640 ASAP na Rihanna

Mon, 25 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mara ya kwanza baada ya kukamatwa kwa rapper ASAP Rocky kufuatia tukio la kufyatua risasi hovyo huko Hollywood, yeye pamoja na Rihanna wamepigwa picha za pamoja.

TMZ inaripoti kuwa wapenzi hao walionekana wakitoka kwenye mgahawa wa Santa Monica Giorgio Baldo usiku wa Jumamosi ya Aprili 23, 2020.

Inasemekana mwimbaji huyo alisherehekea shereheya kumkaribisha mtoto wake ‘baby shower’ akiwa huko, ambayo ilihudhuriwa na familia na marafiki zake wa karibu pekee.

“Walionekana kuwa wenye furaha na utulivu. Rihanna alionekana kupendeza sana. Alikaa karibu na A$AP na walionekana wenye maelewano na upendo mkubwa, walikula kwa masaa kadhaa kabla ya kuondoka katika eneo hilo.” chanzo kiliuambia mtandao wa People.

Licha ya kuzuka kwa sakata la uvumi wa Asap Rocky kumsaliti Rihanna na changamoto ya rapa huyo kutiwa nguvuni na polisi nchini Maarekani bado wawili hao wameonekana kuendelea vizuri pamoja na kuwepo kwa hofu ya Rihanna kushindwa kuhimiliki uzito wa matukio hayo kutokana na hali ya ujauzito aliyonayo..

Asap Rocky aliachiwa huru kwa dhamana ya kiasi cha $550,000 ambacho ni sawa na zaidi ya Bilioni 1.2 za Kitanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live