Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AFANDE SELE ATOA YA  MOYONI KUMHUSU JPM

0793817b9f0c41dcf682e82890c34799 AFANDE SELE ATOA YA  MOYONI KUMHUSU JPM

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MSANII wa Muziki wa Hip Hop na Bongo Fleva kutoka mkoani Morogoro, Seleman Msindi au maarufu Afande Sele amemtaja aliyekuwa Rais wa Tanzania , Dk John Magufuli kuwa alitaka keki ya Dunia igawanywe sawa kwa sawa bila ya upendeleo .

Pia ametoa wito kwa viongozi wanaokuja na waliopo wavivae viatu vya Dk Magufuli kiukweli na si kiunafiki, kwani wapo baadhi ya viongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Serikalini waliona alikuwa akiwababa.

Licha ya baadhi ya viongozi pia wapo baadhi ya matajiri kwa upande wao nao walimchukia kutokana na uamuzi wake wa kuwatetea wanyonge, kwani siku zote matajiri wanapenda kuwatumia watu wanyonge kama mtaji wao .

Afande Sele , alibainisha hayo wakati akizungumza na gazeti hili jana kufuatia kifo cha Dk Magufuli Machi 17 mwaka huu Dar es Salaam.

Msindi, kimuziki amewahi kushinda tuzo ya mkali wa rhymes mwaka 2003 kutokana na wimbo yake wa "Darubini Kali" akiwa na makundi ya 'Ghetto Boys' na 'Watu Pori', yaliyokuwa na makazi yake mjini Morogoro.

Hivyo, alisema Watanzania waliomba na kusali sana kwa zaidi ya miaka 30 ili waweze kumpata Rais ambaye atawatetea watu wanyonge na baada ya kumpata na katika muda mfupi Rais wetu ameondoka kwa mapenzi ya Mungu huyo huyo.

Msanii huyo , alisema ; “ Kuondoka duniani kwa Rais Magufuli ni pigo kwa wale mama mtilie , wamachinga, na watu wanyonge wa nchi hii kwani aliwasaidia sana katika miaka yote mitano.

Machi 15, 2018 Afande Sele alitangaza rasmi kujiunga na CCM mbele ya Rais Dk Magufuli kwa lengo ka kuunga mkono jitihada zake anazozifanya katika kupigania na kukiomba chama kimpokee kama kijana wao.

Afande Sele alieleza hayo wakati alipokuwa anatumbuiza muziki kwa wananchi wa mkoa wa Morogoro walioweza kuhudhuria shughuli za uzinduzi wa kiwanda cha Sigara mkoani humo na Rais Magufuli alikuwa mgeni rasmi.

“Naomba nikupongeze sana kwa hilo lakini kama haitoshi naomba nikuhakikishie kwamba leo hii kutoka kwa dhati ya moyo wangu nimeamua nisimame upande mmoja na wewe ili nisiachwe katika maendeleo,” alisema Afande Sele katika ziara hiyo ya Magufuli.

“Nawaomba viongozi ngazi ya mkoa wa CCM mnipokee kijana wenu nije kuongeza nguvu”, alisisitiza Afande Sele.

Chanzo: www.habarileo.co.tz