Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

A-Z sakata la Nay wa Mitego kumshushia kichapo Calisah

Calisah Na Nay A-Z sakata la Nay wa Mitego kumdunda Calisah

Thu, 21 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama ulipata nusunusu juu ya sakata hili, Tanzaniaweb.com inakuletea undani wake baada ya Calisah mwenyewe kulisimulia mwanzo mwisho.

Iko hivi, wiki kadhaa zilizopita Calisah alikuwa anatoka zake kuangalia muvi akiwa na mpenzi wake (hakumtaja jina) Mlimani City ndipo ishu ilipoanza alipokuwa kwenye maegesho ya magari, jirani na mgahawa wa Samaki Samaki.

Calisah aliwaona baadhi ya wasanii ambao walikuwa wamekaa jirani na SamakiSamaki ndipo alipokwenda kuwasalimia.

“Nilipofika pale alitokea jamaa mmoja ambaye si msanii na simfahamu jina akaanza kumshika mpenzi wangu nywele. Alimshika mara ya kwanza mpenzi wangu akaonekana kutopenda na mimi nikawa namuangalia.

“Akamshika mara ya pili na nikaona tena mpenzi wangu anamfokea. Nikajaribu kumuonya kwamba hata kama wanafahamiana basi pale aheshimu sababu mimi ndiyo nimekwenda naye,” anasema Calisah.

Calisah amezidi kueleza kuwa, baada ya kurudia mara nyingine na alipomuonya jamaa akaonekana kumtukana tusi kubwa ndipo alipomtia ngumi moja ya nguvu na kumpasua palepale akaanza kutoka damu.

Wakati anaondoka eneo hilo, ndipo Nay wa Mitego alipotokea na kwa vile anamfahamu alifikiri amekwenda kumuuliza nini kimetokea lakini badala yake akashangaa kuona naye anamsukuma chini.

“Alinisukuma nikaanguka chini akiwa na kampani yake. Kisha akanikanyaga usoni mara mbili. Nilipoinuka, wakaja baadhi ya wasanii ninaowafahamu wakanishika lakini niliwaambia kwa nini wananishika mimi badala ya Nay ambaye amenipiga?

“Basi nikawa mpole nikajifanya naondoka lakini sikukubali nikamfukuza hadi Sinza Studio kwake lakini sikufanikiwa kumkuta ndipo niliposhauriwa kwenda kuchukua RB,” anasema Calisah.

Jamaa huyo anasema baada ya kuchukua RB, siku moja alipata taarifa kuwa Nay anashuti na Aalikiba ndipo alipofika eneo hilo akiwa na polisi kumkamata.

“Ilitokea vurugu pale na alikutwa na vitu ambavyo siwezi kuvitaja visije vikazidi kumtia matatizoni maana hakuwa hata na vibali. Sakata likawa kubwa, simu zikapigwa sana na bahati yake MwanaFA alinieleza nimsamehe.

“Tulikubaliana liishe pale waendelee kushuti lakini afike polisi siku inayofuata. Jamaa hakufika na hata wiki ikapita hakutokea polisi. Mimi sitaliacha hili suala, nitalifatilia hadi kieleweke.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live