Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

5G yapigwa 'Stop' Marekani

C Z VOHUFb9V9Emsscc33n7pV Kt7cwEs7kroOXrrX6myZ7bhlIDTtaWjfNLoz3vfFA5RTFx C3OH8ukZMdK4tKqMgSCd4FAZYTe 5G yapigwa 'Stop' Marekani

Mon, 3 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Marekani imetoa wito wa kutaka kucheleweshwa kwa shughuli ya usambazaji wa mtandao wa kasi ya 5G kwenye simu za mkononi kutokana na uwezekano kuathiri usafiri wa anga.

Waziri wa Uchukuzi Pete Buttigieg na Mkuu wa Usimamizi wa Anga (FAA), Steve Dickson wametoa wito kwa waendeshaji wa mitandao wa AT&T na Verizon kuahirisha kwa wiki mbili uzinduzi wa mtandao huo uliopangwa kufanyika Januari 5.

FAA inahofia teknolojia ya 5G inaweza kuingilia utendaji kazi wa vifaa fulani vya kieletroniki vya ndege, na kuongeza kuwa masafa yanayotumika na mtandao wa 5G nchini Marekani yanakaribia kufanana na masafa yanayotumika katika altimita za ndege.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live