Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

50 Cent muziki, filamu vinampa maisha

5O Cent Maisha 50 Cent muziki, filamu vinampa maisha

Tue, 9 Apr 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Katika sakata la kutafutwa kwa P Diddy, mmoja kati ya watu walioonekana kufurahishwa na suala hilo ni rapa Curtis Jackson ‘50 Cent’ ambaye alitumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kuandika vijembe mbalimbali na amekuwa akiwafanyia kebehi mastaa karibu wote wanaoingia matatani na mamlaka za kisheria akiwamo R.Kelly.

Licha ya mambo yake hayo, rapa huyu ni mmoja kati ya wasanii wenye pesa Marekani ingawa kuna kipindi alifilisika.

Hadi sasa anakadiriwa kuwa na utajiri unaofikia Dola 40 milioni na leo tumekusogezea uone jinsi alivyoupata utajiri wake na jinsi anavyopiga pesa.

ANAPIGAJE PESA

Ana utajiri unaokadiriwa kufikia Dola 40 milioni. Kiasi hicho cha pesa kimetokana na pesa ambao alizipata kupitia shughuli mbalimbali kuanzia muziki wake na biashara nyingine.

50 Cent alipata pesa nyingi kupitia hisa zake katika kampuni ya Glaceau ambayo ilikuwa ikijihusisha na utengenezaji wa maji ya Vitamini.

Pesa hizo alizipata baada ya Coca-Cola kuinunua Glaceau mwaka 2007 kwa Dola 4.1 bilioni, yeye alikuwa na asilimia mbili ya hisa na kwenye mgao alipata kati ya Dola 100 milioni hadi Dola 150 milioni.

Mabadiliko ya 50 Cent kutoka kuwa rapa maarufu hadi kuwa mzalishaji wa filamu na tamthilia mwenye mafanikio, yamemtajirisha sana akiandaa vipindi vya televisheni ambavyo vinapendwa Marekani kote. Alianza kuingia katika soko la filamu mwaka 2003 alipoanzisha kampuni yake ya G-Unit Films, ambayo baadaye ikashirikiana na cable network ya Starz kuandaa kazi kadhaa ikiwamo tamthilia iliyotamba zaidi ya Power iliyoenda kwa misimu sita kuanzia 2014-2020. ‘Mume’ wa Vanessa Mdee, Rotimi Akinosho amepata umaarufu katika tamthilia hii ya Power.

Mwaka 2015, 50 alitangazwa kuwa amefilisika kutokana na madeni mbalimbali yaliyokuwa yanamuandama likiwamo lile la Dola 5 milioni lililosababishwa na kesi kuachia picha za utupu za demu wa zamani wa rapa Rick Ross, Lavonia Leviston.

Kwa sababu hiyo alilazimika kuuza hisa zake za kampuni ya Effen Vodka ambapo anakadiriwa kwamba aliingiza Dola 60 milioni.

Ilipofika Oktoba 2018, alisaini mkataba wa miaka minne na kampuni ya Starz, kwa ajili ya kuhusika katika kipindi maalumu cha televisheni. Dili hilo lilikuwa na thamani ya Dola 150 milioni.

Kupitia muziki 50, anakadiriwa kuingiza zaidi ya Dola 100 milioni kupitia shoo na uuzaji wa albamu zake.

NDINGA

Maserati MC12-Dola 810,000

Bugatti Chiron-Dola 2.9 milioni

Bentley Mulsanne-Dola 335,000

Lamborghini Aventador S Roadster- Dola 460,247

Rolls-Royce Cullinan- Dola 391,750

Mercedes G500 (2018)-Dola 199,900

Ferrari FF-Dola 618,420

Rolls Royce Drophead-Dola 500,000

MSAADA KWA JAMII

Ana taasisi yake iitwayo G-Unity Foundation ambayo inajihusisha na kusaidia watoto waishio maeneo ya vijijini katika nchi ya Marekani.

Taasisi hii hasa imejikita kwenye kutoa misaada ya kielimu. Yeye ndio mmiliki ingawa alianzisha kwa kushirikiana na wasanii wengine wa kundi lake la G-Unit.

MIJENGO

Rapa huyu anaishi New York City na Hustpoon ambako kote anadaiwa kuwa na nyumba zinazofikia thamani ya Dola 5 milioni kwa ujumla.

Aliwahi kuwa na mjengo wa kifahari sana huko Connecticut, nyumba hiyo ambayo aliiuza kwa Dola 2.9 milioni mwaka 2019, aliinunua kwa Dola 4.1 milioni kutoka kwa aliyekuwa mke wa Mike Tyson, Marc Tuner.

BATA NA MAISHA BINAFSI

Kwa sasa yupo kwenye uhusiano na mrembo Cuban Link, ambaye pia ni rapa kutoka kundi la Terror Squad.

Kwenye upande wa watoto anao wawili wa kiume kwanza akiwa ni Marquise Jackson, aliyezaa na Shaniqua Tompkins mwaka 1996, wa pili ni Sire Jackson, aliyezaliwa na aliyekuwa mchumba wake Daphne Joy mwaka 2012.

Chanzo: Mwanaspoti