'Bifu' la East Coast na West Coast, ambalo lilipelekea vifo vya rapa Tupac na Notorious BIG, kama ulidhani limeisha basi ndo kwanza linaanza kutaradadi tena.
Wakati maafisa wa polisi Marekani wakipewa kibali cha kumtia nguvuni Diddy, kwa tuhuma za unyanyasaji wa kingono, rapa 50 Cent kajitokeza na kukazia shutuma hizo kwa mamilioni ya 'fansi' wake mitandaoni.
Kupitia ukurasa wake wa X 50 Cent aliandika kuwa, "Sasa hivi siyo Diddy kafanya ni Diddy kamalizwa, hawajui hivyo isipokuwa wamepata kesi."
Hii siyo mara ya kwanza 50 Cent 'kumdisi' mwana hadharani kwani katika baadhi ya mahojiano ambayo kawahi kufanya na Breakfast Club, alisema Diddy sio mtu mwema kama watu wanavyodhania.