Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

50 Cent anaota kuwa Mfalme wa New York?

50 X Jay X X Diidy 50 Cent anaota kuwa Mfalme wa New York?

Fri, 29 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Ni swali linalozunguka sana kichwani kwangu kwa muda sasa. Ni baada ya kushuhudia yanayoendelea katika ardhi iliyo chini ya namlaka ya Joe Biden, Marekani.

Bilionea Diddy anasakwa kama 'Osama wa Kizazi Kipya'. Kwa madai ya ugaidi wa unyanyasaji wa kingono. Na muhusika mkuu ni Cassie, pisi iliyowahi kumiliki mbavu za Diddy hapo kabla.

Hakuwa mpita njia kwake bali alikuwa mchumba. Ni mmoja wa warembo waliowahi kuwa sehemu ya maisha yake. Mwana kaingia mitini. Kasepa mbele ya viumbe wenye nyota kadhaa za uwezo mkubwa wa msako.

Wakati hayo yakiendelea. 50 Cent naye amekuwa na dunia yake ya 'kudisi'. Anawasha moto kila siku mbele ya mamilioni ya wafuasi wake mitandaoni. Akiamka ni Diddy, akilala ni Diddy. 'Anamdisi' msela wa New York kunakuchwa mpaka machweo.

Hivi sasa 50 kapanda ngazi. Siyo Diddy tu, kamuingiza na bilionea mwingine wa muziki Jigga Man. Anawataja kama watu wasiyo wasafi. Wenye makandokando kama Diddy, na mmoja wapo ndo huyo Jay Z.

50 Cent kaanza kitambo kumchana Diddy, kuwa siyo mtu safi, kama wengi wanavyomuona. Na pengine akaenda mbali kwa kumtaja kama muhusika wa kifo cha Tupac Amaru Shakur.

Licha ya 50 Cent kutokea upande wao hao anaowataja. Yaani New York 'East Coast'. Ni kama hajali ule 'uhomu boi' wao kabisa. Sasa swali ni: Je, 50 Cent 'tageti' yake ni nini? Kwamba ana uchungu sana na kina Cassie au anautaka ufalme wa New York?

Chanzo: Mwanaspoti