Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

50 Cent amshitaki daktari kuhusu kuongeza uume wake

50 Cent Hnm.jpeg 50 Cent

Sun, 18 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rapa maarufu nchini Marekani Curtis James Jackson III '50 Cent' amefungua kesi dhidi ya daktari bingwa wa upasuaji baada ya kuripotiwa Hospitali yake Imetumia picha yake kudai kuwa alikuwa mmoja wa wateja wao.

Rapa huyo anamshitaki daktari bingwa wa upasuaji wa plastiki Angela Kogan na kampuni zake, Perfection Plastic Surgery na MedSpa, akieleza kuwa wanaendelea kutumia picha yao ya zamani wakiwa pamoja na kudai alifanyiwa upasuaji wa kuongeza uume.

Picha hiyo ilichukuliwa mnamo Februari 2020 baada ya 50 Cent kupiga picha na mtu aliyedhani ni shabiki ila sasa anaitumia picha kukuza biashara zake.

50 anasema alikuwa na wasiwasi baada ya chanzo kingine cha habari kuchapisha makala na Dk. Krogan kuhusu upasuaji na kuongeza nguvu za kiume.

Nakala hiyo ilikuwa na picha ya Krogan na 50 Cent mnamo Agosti. Stori imefutwa Online ila bado ipo kwenye Search Engines.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live