Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

15 kutoa ushahidi kesi dhidi ya Idriss

IDRISSS 15 kutoa ushahidi kesi dhidi ya Idriss

Fri, 10 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

UPANDE wa Jamhuri umesema unatarajiwa kuita mashahidi 15 dhidi ya msanii Idriss Sultan (27) na Innocent Maiga, wanaokabiliwa na kesi ya kushindwa kusajili laini ya simu inayomilikiwa na mtu mwingine.

Kesi hiyo imepangwa kuanza kusikilizwa ushahidi Agosti 5, mwaka huu.

Awali, mahakama hiyo iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashidi Chaungu, ilisikiliza maelezo ya awali ya washtakiwa. Wakili wa Serikali, Silvia Mitanto, alidai kuwa kesi hiyo imepangwa kwa ajili ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali.

Alidai kuwa kati ya Desemba Mosi, 2019 na Mei 19, 2020 katika eneo la Mbezi Beach, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Idriss alitenda kosa la kushindwa kufanya usajili wa laini ya simu inayotumiwa na mtu mwingine.

Ilidaiwa kuwa katika kosa hilo mshtakiwa alitumia kadi ya simu iliyomilikiwa na Innocent Maiga bila kuripoti kwa mtoa leseni.

Katika shitaka la pili, mshtakiwa Maiga anadaiwa kutenda kosa la kushindwa kutoa taarifa ya mabadiliko ya kadi ya simu kutoka kwake kwenda kwa Idriss, kosa analodaiwa kulitenda kati ya Desemba Mosi, 2019 na Mei 19, mwaka huu, eneo la Mbezi Beach, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Pia alidai Mei 5, mwaka huu, Mkuu wa Upelelezi Kinondoni, alipewa taarifa kwamba Idriss anatumia kadi ya simu ya Vodacom ambayo haijasajiliwa kwa jina lake na kwamba alitakiwa kuripoti Kituo cha Polisi Oysterbay na alifanya hivyo.

Ilidaiwa polisi walienda kufanya upekuzi nyumbani kwa Idriss na kubaini uwapo wa laini hiyo ya simu aliyokuwa akiitumia kwa mawasiliano yake ya kila siku licha ya kusajiliwa kwa jina la Maiga.

Ilidaiwa Idriss aliakiri kutumia kadi hiyo ya simu ambayo ilikuwa ikimilikiwa kabla na Maiga na kwamba alikiri kuitumia tangu Desemba, mwaka jana.

Maiga alidaiwa kukiri kumiliki kadi hiyo na alimpatia Idriss aweze kuitumia na alikiri kutoripoti kwenye mamlaka kuhusu mabadiliko ya kadi hiyo.

Upande wa mashtaka ulidai utaleta mashahidi 15.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live