Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

100,000 washiriki tamasha la Jamafest

77677 TAMASHA+PIC

Sat, 28 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Leo Jumamosi Septemba 28, 2019 ndio kilele cha tamasha la nne la Jumuiya ya Afrika Mashariki Utamaduni Festival (Jamafest) linalofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Suzan Mlawi amesema katika tamasha hilo la nne wametembelewa na wageni mbalimbali wasiopungua 100,000.

Mlawi amesema mbali ya waliofika hapo kwenye viwanja vya Duce na Uwanja wa Taifa  walitembelea na watu  milioni tatu kupitia mitandao ya kijamii.

 "Leo siku ya nane ndio kilele cha Jamafest tumepata mafanikio kama ambavyo takwimu za waliotembelea moja kwa moja na kwenye mitandao ya kijamii, " amesema Mlawi.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz