Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zitto Kbawe atinga Kisutu kesi ya Mbowe

ZITOOOO Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu ACT

Fri, 6 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ni miongoni mwa Watu waliofika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu muda huu kufuatilia mwenendo wa kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.

Ikiwa ni siku mbili zimepita tangu viongozi wa vyama vya upinzani kukutana na Balozi wa Marekani Victoria Nuland, kujadili mwenendo wa siasa nchini, hatua hii ya Zitto inaamsha ari ya Umoja kwa vyama vya upinzani nchini.

Zitto ni miongoni mwa wanasiasa waliowahi kushtakiwa kwa makosa tofauti tofauti ya kisiasa katika awamu za uongozi zilizopita. Ikiwa ni pamoja na kupokea kifungo cha mwaka mmoja cha kutotumia mitandao ya kijamii kuongea mambo yanayohusu dola kwa ujumla.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live