Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yamkuta baada ya kutumia pesa za muamala uliokosewa kununua mjengo

Nyumba Crypto Yamkuta baada ya kutumia pesa za muamala uliokosewa kununua mjengo

Thu, 1 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke mmoja kutoka eneo la Melbourne nchini Australia aitwaye Thevamanogari Manivel yamemkuta baada ya kutakiwa kulipa kiasi cha dola za Kimarekani zaidi ya milioni 9 (zaidi ya Tsh bilioni 16) kwa kampuni ya CRYPTO ya nchini Singapore baada ya kampuni hiyo kumuwekea fedha hizo kwenye akaunti yake ya benki kimakosa.

Imeelezwa kuwa, baada ya kuziona pesa hizo kwenye akaunti yake, Manivel alikaa kwa muda wa miezi saba bila kuzigusa, lakini baada ya kuona muda mrefu umepita pasi na mtu yoyote kujitokeza kuzidai alimua kuzitoa na kununua nyumba ya ndoto zake huku fedha nyingine akizitawanya kwenda kwenye akaunti za ndugu zake sita.

Manivel alitumia dola laki 9 za Kimarekani ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 2 kununulia nyumba hiyo yenye vyumba vitano ambapo baada ya hiyo miezi saba Kampuni hiyo iligundua makosa hayo na kuanza taratibu za kisheria mwezi Februari na kumfungulia mashitaka ya kutaka alipe pesa zote pamoja na riba.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Victoria nchini Australia, James Elliott licha ya kuamuru kulipwa kwa fedha hizo alishangazwa na walalamikaji kwa kutotambua makosa hayo ya malipo kwa muda wa miezi saba ambapo hata hivyo aliagiza Manivel kulipa fedha zote ikijumuisha asilimia 10 ya riba na ada za kisheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live