Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Willy Paul, Diana Marua Wafikishana Pabaya

Willy Paul Diana Willy Paul, Diana Marua Wafikishana Pabaya

Thu, 30 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MAHAKAMA nchini Kenya imemuagiza mtayarishaji wa maudhui ya Televisheni na mwimbaji kutoka nchini Kenya Diana Marua kufuta video yake aliyoiweka kwenye channel yake ya mtandao wa YouTube akimshutumu mwanamuziki Willy Paul kuwa aliwahi kujaribu kumbaka.

Kulingana na agizo lililotolewa na Hakimu Mkuu Mwandamizi D.W Mburu Desemba 29, 2021, Diana alizuiwa kutoa madai yoyote zaidi kuhusu Willy Paul licha ya kumshutumu vikali kwa tuhuma zilizopeleka kuzua taharuki kote Mitandaoni.

"Inaamriwa kuwa video ya mshtakiwa/mlalamikiwa na chapisho la mtandao wa kijamii lililowekwa kwenye chaneli yake ya YouTube yenye jina la 'My untold story', Willy Paul alijaribu kunibaka, liondolewe kusubiri kusikilizwa na kuamuliwa kwa shauri hili kwa vile linamkandamiza mlalamikaji/ mwombaji na kumfanya apoteze fursa mbalimbali ikiwamo za kibiashara na kumfanya ateseke kiafya."

“Kwamba mshtakiwa/mlalamikiwa humu ndani aidha yeye mwenyewe, watumishi wake, mawakala, kazi au mtu mwingine yeyote anayesambaza video hiyo anazuiliwa kwa amri ya muda ya mahakama dhidi ya kukashifu, kueneza na kuendelea kumchafua mlalamikaji/mwombaji. Ikisubiri kusikilizwa na kuamuliwa kwa shauri hilo,” yalisomeka maagizo hayo ya hakimu.

Kesi hiyo ilifikishwa mahakamani na mwanamuziki kutoka nchini Kenya Willy Paul punde baada ya kushutumiwa kwa kesi ya kutaka kujaribu kumbaka mtayarishaji wa maudhui na muimbaji Diana Marua.

Ambaye alikitumia kipindi chake kinachoruka kupitia chaneli yake ya Youtube kutamka maneno hayo yaliyozua gumzo kubwa huku malalamiko ya mashabiki yakielekezwa kwa msanii Willy Paul.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live