Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wilaya 50 kupata ofisi za mashitaka

Hukumu Pc Data Wilaya 50 kupata ofisi za mashitaka

Mon, 24 Apr 2023 Chanzo: Habarileo

SERIKALI imetoa kibali kwa kufungua ofisi mpya katika wilaya 50 za Tanzania Bara ili kusongeza huduma kwa ukaribu na uharaka zaidi kwa wananchi.

Mkurugenzi wa Mashitaka, Sylvester Ofisi ya Taifa ya Mashitaka iajiri watumishi 353 mwaka huu wa fedha hivyo kuiwezesha.

Mwakitalu alisema hayo mjini Morogoro wakati akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Naibu Wizara ya Katiba na Sheria, Pauline Gekul kufunga mafunzo elekezi ya awali kwa waajiriwa wapya 216 wa Ofisi ya Taifa ya Mashitaka.

Watumishi hao ni waendesha mashitaka, makatibu sheria na mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo ili kuwawezesha kufahamu namna ya kuenenda na kufanya kazi wakiwa ni watumishi wa serikali yaliyendeshwa na wakufunzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania tawi la Singida.

Mwakitalu alisema kabla ya kupata watumishi wapya, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ina ofisi 43 ambazo zipo kwenye makao makuu ya mikoa yote 26 na nyingine katika wilaya ambazo wadau wao wanazo kanda maalumu.

Alisema mkoa wa Dar es Salaam katika wilaya zake wadau wao wameiweka ni mikoa ya kipolisi ambayo ni Temeke, Ilala, Kinondoni na mkoa mwingine wa kipolisi ni Tarime na Rorya na yote hiyo imekuwa na ofisi za mikoa za mashtaka.

Alisema kutokana na utaratibu huo idadi ya ofisi za mikoa ni 30 wakati kwa wilaya ni 13 na hivyo kuifanya ofisi ya taifa ya mashtaka kwa nchi nzima kuwa na ofisi 43.

Mwakitalu alisema kupatikana kwa kuwapata watumishi wapya 353, hivi sasa wanaouwezo kufungua ofisi katika wilaya 50 na kuzihudumia kikamilifu zaidi.

“Namshukuru Rais wetu kwa kutoa kipaumbele kwa ofisi yetu kupata kibari cha kuajiri watumishi hawa wakutosha si rahisi, ni jambo kubwa sana na kwa kitendo hiki sisi tunahidi sasa tutawahudumia watanzania katika eneo hili la mashtaka kikamilifu,” alisema Mwakitalu.

Mwakitalu alisema, ofisi za wilaya hizo mpya zitaanzishwa siku chache zijazo na zitaanza kutoa huduma kwa wananchi Mei Mosi mwaka huu.

Alisema baada ya kuanzishwa kwa ofisi katika wilaya hizo mpya, wafakuwa wamezifikia wilaya 93 na endapo watapata watumishi wengine wapya, wilaya zote ambazo zina Mahakama ya wilaya zitafikiwa.

Kwa upanda wake, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Gekul katika hotuba yake aliwataka waajiriwa wapya waliopatiwa mafunzo hayo kuwa na uweledi, kuepuka vitendo vya ukiukaji wa maadili ya kazi, kuepuka rushwa, uonevu na matumizi mabaya ya ajira zao.

Naibu Waziri aliwataka wazingatie misingi ya kusimamia sheria bila kumwonea mtu wala kumpendelea mtu yeyote wakati wa utendaji wao wa kazi ili kuhakikisha haki inapatikana kwa usawa.

Chanzo: Habarileo